Idara ya Habari na Mawasilino ya Klabu ya Simba SC imekiri kukosea jina la timu waliocheza nayo juzi Jumamosi (Julai 23) katika mchezo wa Kimataifa wa Kirafiki wakiwa Kambini nchini Misri.
Simba SC iliripoti katika kurasa zake za Mitandao ya Kijamii imecheza dhidi ya Al Okhdood na kuicharaza bakora 6-0 katika mchezo huo.
Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally amekiri kuna makossa ya kiuandishi yalifanywa katika Kurasa zao za Mitandao ya Kijamii, hivyo wameomba radhi kwa makossa hayo.
“Tunaomba radhi kwa klabu ya Al Okhdood, ni makosa madogo ya kiuandishi yalitokea”
“Kulikuwa makosa kidogo ya kiuandishi ni kweli hatujacheza na Al-Okhdood Club bali tumecheza na “Abou Hamad” (Matamshi yake) kwa hiyo ni kosa tu kidogo la kiuandishi maana Al-Okhdood Club ipo kwenye list ya timu tutakazocheza nazo” amesema Ahmed
Kuhusu maendeleo ya Kambi ya kikosi chao huko Ismailia-Misri, Ahmed amesema jana Jumapili (Julai 24) kikosi chao kilipumzishwa kufuatia Kocha Mkuu Zoran Maki kutoa nafasi hiyo kwa wachezaji wake, na leo Jumatatu (Julai 25) kimeendelea na maandalizi ya kuelekea msimu mpya wa 2022/2023.
“Jana Jumapili hatukufunya mazoezi, kocha ‘Zoran’ aliwapa mapumziko wachezaji, leo ‘Jumatatu’ tunarejea mazoezini”
“Tutacheza Mchezo wa kirafiki Jumamosi, tutawajuza ni timu ipi tutacheza nayo” Amesema Ahmed Ally
Tayari Simba SC imeshacheza michezo miwili ya kirafiki, ikitoa sare ya 1-1 dhidi ya Ismailia FC na juzi Jumamosi ilishinda mabao 6-0 dhidi ya Abou Hamad.