Mlinda Lango Mkongwe nchini Tanzania Juma Kaseja Juma bado ataendelea kuwa sehemu ya kikosi cha KMC FC kwa msimu ujao wa Ligi Kuu na Michuano ya Kombe la Shirikisho ‘ASFC’.

Awali Mlinda Lango huyo aliyewahi kuvitumikia vilabu vya Simba SC, Young Africans, Kagera Sugar na Mbeya City, alitajwa huenda angekua sehemu ya wachezaji wanaoachwa katika kipindi hiki cha usajili.

Baada ya kusambaa kwa tetesi hizo kuhusu Mlinda Lango huyo, uongozi pamoja na Kaseja wametoka hadharani kukanusha taarifa na kuthibitisha kuwa Mkongwe huyo bado ataendelea kuwa kwenye kikosi cha timu hiyo kwa msimu ujao.

Katibu Mkuu wa KMC FC Walter Harrison amesema, Kaseja bado ni mchezaji wa klabu hiyo na amekuwa mfano ndani ya timu hivyo, hivyo wataendelea kuwa naye kwa maslahi ya timu na wachezaji chipukizi.

“Wapo wachezaji ambao tumewaacha lakini Juma bado yupo sana KMC hata kama hatakuwa mchezaji lakini tutamtafutia hata nafasi nyingine.” amesema Walter Harrison

Kwa zaidi ya muongo mmoja Kaseja amekuwa Mlanda Lango Mzawa mwenye ubora wa hali ya juu, licha ya kwamba kwa msimu uliopta hakupata nafasi ya kucheza mara kwa mara katika kikosi cha kwanza cha KMC FC.

Klabu hiyo inayomilikiwa na Manispaa ya Kinondoni, tayari imeshatangaza kuachana Malinda Lango kutoka Kenya Farouk Shikalo anayedaiwa kujiunga na Mtibwa Sugar.

James Kotei aongeza miwili Singida Big Stars
Prof. Ndalichako asimama na madereva