Serikali imeonya Wamiliki wa Vyombo vya Usafirishaji nchini kutojaribu kuwashushia posho madereva wao baada ya kupangwa kwa viwango vya chini vya posho hizo.

Taarifa ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako imesema baadhi ya wamiliki wanakusudia kushusha viwango vya posho vya awali ambavyo viko juu ya wastani wa posho iliyokubaliwa kati ya Serikali, Madereva na Wamiliki wa vyombo vya usafiri.

“Kama mnavyokumbuka mnamo tarehe 22 Julai, 2022 Serikali ilitoa taarifa kwa Vyombo vya Habari kuhusu hatua zilizochukuliwa katika kushughulikia Hoja na Malalamiko yaliyowasilishwa na Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi Madereva na Wamiliki wa Vyombo vya Usafirishaji nchini,” alisema Prof. Ndalichako.

Ameongeza, ”Kufuatia kutolewa kwa taarifa hiyo, wapo baadhi ya Madereva ambao wameipokea kwa mtazamo tofauti. Kutokana na hali hiyo, wamekuwa wakipotosha taarifa hiyo na kuchochea ama kuhamasisha Madereva wenzao kugoma. Uchochezi wa mgomo wao umejikita katika viwango vya posho ambavyo Madereva, Wamiliki wa Vyombo vya Usafiri na Serikeli waliafikiana katika vikao vya majadiliano,” amesema Waziri Ndalichako.

Viwango ambavyo vimekubaliwa ni viwango vya chini vya posho za safari (Minimum allowances) ambapo waajiri hawaruhusiwi kulipa chini ya viwango hivyo.

Uongozi KMC wamkingia kifua Juma Kaseja
Makamba ataka uaminifu Wakandarasi wazawa