Ndugu wanachama, mashabiki wa Simba na Watanzania wenzangu, Nchi yetu tuipendayo ya Tanzania inafanya uchaguzi tarehe 25 Oktoba 2015.

Kwa niaba ya Uongozi wa Simba tunapenda kuwatakia Watanzania wote Uchaguzi mwema. Amani, ni tunu tuliyopewa na Mungu na pia Waasisi wa Taifa hili, hivyo ni jambo la muhimu mno kuitunza na kuienzi.

Amani na Umoja ndio msingi muhimu wa maendeleo sio tu wa kiuchumi bali pia mpira wa miguu.

Napenda kumalizia kwa kuwashukuru kwa kuendelea kuishangilia timu yenu.

Evans Aveva

Rais wa Simba

Chanzo: http://simbasports.co.tz

 

Updates: Alichokisema J Makamba kuhusu ‘taarifa za chopa ya CCM kuanguka’
Wachezaji Wa Eritrea Watokomea Botswana