Meneja wa klabu ya Manchester City, Pep Guardiola amesema atafanya mazungumzo na beki John Stones mwishoni mwa msimu huu ili kujua hatma ya mchezaji huyo kama atasalia au ataondoka Etihad Stadium.

Stones raia wa England amekua akisumbuliwa na majeruha ya mara kwa mara toka ajiunge na klabu hiyo ya mjini Manchester City akitokea Everton mwaka 2016, hali inayosababisha akose nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza.

Kukosekana kwa utimamu wa mwili wa Stones kunasababisha ashindwe kuwania nafasi kwenye safu ya ulinzi ambayo ina wachezaji wengi wenye ubora kama Aymeric Laporte, Eric Garcia, Nicolas Otamend na Fernandinho.

Imeripotiwa kuwa mkataba wa beki huyo utamalizika mwaka 2022 na tayari klabu za Arsenal na Everton zimeonesha nia ya kuhitaji huduma yake.

Msimu huu Stones amecheza michezo 20 katika michuano yote (12 ya Ligi Kuu) kutokana na kusumbuliwa na majeruhi ya kifundo cha mguu.

Msimamo wa Kocha Sven wavuruga mipango Simba SC
Picha: Simba SC watua Dar es salaam