Mamlaka ya utawala wa kijeshi nchini Sudan, imeamuru masomo kuahirishwa na shule kufungwa nchi nzima kutokana na maandamano yaliyoibuka baada ya kuuawa kwa kupigwa risasi baadhi ya wanafunzi wakati wa maandamano katika jimbo la kordofan.
Katika maandamano hayo yaliyolenga malalamiko kwenye sekta ya mafuta na upungufu wa mkate, licha ya wanafunzi wanne kupoteza maisha na mwanachi mmoja, watu kadhaa walijeruhiwa baada ya risasi kufyatuliwa kiholela.
Idara ya uhamiaji yatoa ufafanuzi kuhusu Mwandishi aliyekamatwa
Kwamujibu wa taarifa iliyotolewa na shirika la habari la Suna, Mamia ya wanafunzi waliovaa sare za shule waliandamana jana wakiwa wanapunga bendera za nchi yao kudai haki ya wenzao waliouawa na kupelekea mamlaka kuamuru magavana wa majimbo yote kufunga shule zote mpaka yatakapotolewa maelekezo mengine.
Kangi Lugola ang’aka, ‘Hatuwezi kurudi utumwani tena’
Shirika la umoja wa mataifa linalohudumia watoto duniani, Unicef, limeitaka mamlaka nchini Sudan kufanya uchunguzi kuhusu mauaji yaliyotokea na kuhakikisha waliohusika wanafikishwa kwenye mkono wa sheria.
RC Wangabo ataka ukarabati wa Meli ya MV Liemba uharakishwe
Mwenyekiti wa baraza la kijeshi nchini Sudan, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, amekemea mauaji hayo.
“Kilichotokea katika eneo la al-Obeid ni cha kuhuzunisha, kitendo cha kuwaua raia waliokuwa wakiandamana kwa amani ni uhalifu ambao haukubaliki ambao unahitaji hatua za haraka kuchukua” alisema Jenerali Fattah.
Sitashangaa waziri huyu akipita bila kupingwa 2020- Dkt. Bashiru Ally
Video: MacLeans BeneCIBO yawaneemesha wakulima kimasoko