Yoshihide Suga amechaguliwa kuwa kiongozi wa chama tawala cha Liberal Democratic party (LDP) cha nchini Japan.
Hatua ya uchaguzi inamfungulia njia kuchukua nafasi ya Shinzo Abe kuwa waziri mkuu wa nchi hiyo.
Suga ameshinda kwa urahisi kura ya ndani na kutarajia kuchagua mrithi wa waziri mkuu Shinzo Abe, ambaye mwezi uliopita alitangaza kuwa ataondoka madarakani kwa sababu ya matatizo ya kiafya .
Suga ameshinda baada ya kupigiwa kura 377 za ndiyo kati ya kura 534 dhidi ya wagombea wengine wawili, waziri wa zamani wa mambo ya nje Fumio Kishinda.
Kwa kuzingatia idadi kubwa ya wabunge wa LDP, Suga anatarajiwa kupigiwa kura ya bunge mnamo jumatano.