Baada ya Mwanasiasa wa Uingereza, Rishi Sunak kuchaguliwa kuwa kiongozi wa Chama cha Conservative, hatua ambayo inampa nafasi ya kuwa Waziri Mkuu ajaye, baadhi ya watu wamemtaka kuimarisha njia kuu za kiuchumi.
Sunak, atakuwa ni Kiongozi wa kwanza wa taifa hilo asiye Mzungu huku Mfalme Charles III akitarajiwa kumuomba kuunda serikali, na kuchukuwa nafasi ya Liz Truss, aliyejiuzuru baada ya siku 44 za uhudumu wake.
Mpinzani wake aliyejiondoa katika kinyang’anyiro hicho, Penny Modaunt amesema ushindi wa Sunak ni wa kihistoria, ambao kwa mara nyingine umeonyesha uanuwai na kipaji ndani ya chama cha Conservative.
Sunak, sasa anachukuwa nafasi hiyo kufuatia kipindi cha mtikisiko mkubwa wa kisiasa kuwahi kushuhudiwa katika historia ya Taifa la Uingereza.
Naye Mwenyekiti wa chama cha Conservative, Jake Berry ametoa wito wa kushikamana, kumuunga mkono Rishi na kumpa mbinu za kuimarisha njia kuu za uchumi.