Kuelekea maadhimisho ya miaka 46 ya Chama Cha Mapinduzi ‘CCM’, Mkoa wa Tanga utashuhudia tukio la kihistoria la kuashwa taa za Uwanja wa Mkwakwani.

Siku hiyo pia, Coastal Union ‘Wagosi wa Kaya’ na African Sports ‘Wana Kimanumanu’ watacheza mchezo wa kirafiki uwanjani hapo, kuanzia saa mbili usiku.

Tukio hilo ambalo litapambwa na mambo mbalimbali, linatarajiwa kushuhudiwa na Mashabiki wa klabu hizo nguli mkoani Tanga, ambao wataongozwa na Mgeni Rasmi Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ‘SMZ’ Hemmed Abdullah.

Hatua ya klabu hizo kukutana katika mchezo wa Kirafiki itakumbushia enzi za mwaka 1988, ambapo Coastal Union ilitwaa ubingwa wa Tanzania bara, huku African Sports ikitwaa Kombe la Muungano.

Itakumbukwa kuwa msimu uliopita katika michuano ya Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’, Miamba hiyo ilikutana hatua za awali na Coastal Union ilisonga mbele.

Tanzania yaridhia uenyeji mkutano Haki za Binadamu na Watu
Azam FC kuipima Al Hilal Azam Complex