Timu ya ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, jana iliivaa Uganda katika mchezo wa Mzunguuko watatu wa kuwania kufuzu ushiriki wa Fainali za Mataifa ya Bara la Afrika ‘AFCON 2023’ zitakazofanyika mwakani nchini Ivory Coast.

Stars sasa inajiandaa kuwakaribisha majirani zao hao kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam Jumanne (Machi 28) katika mchezo wa Kundi F. ambalo linaongozwa na Algeria yenye alama tisa baada kucheza michezo mi tatu.

Mchezo wa jana Ijumaa (Machi 24) ulichezwa kwenye Uwanja wa Suez Canal, uliopo mji wa Ismailia, Misri baada ya Shirikisho la Soka la Barani Afrika ‘CAF’  kuamua kwamba viwanja vya nchini Uganda kwa sasa haviko katika ubora unaohitajika kuchezewa michezo hiyo.

Mchezo wa jana umeshapita, tunachopaswa kutambua ni kwamba bado kuna michezo mitatu ya hatua hii tukianza na mchezo wa Jumanne dhidi ya Uganda. Hii ina maana kuna alama tisa za kuwania ambazo tukizipata maana yake tutasonga mbele.

Hatua tuliyopo sasa inahusisha makundi 12 ambayo timu mbili za juu kutoka katika kila kundi zitafuzu kucheza fainali hizo za 34 za Mataifa ya Afrika zinazoandaliwa na CAF, ambazo mara hii zitashirikisha mataifa 24. Pia Fainali za Ivory Coast zitakuwa za pili kufanyika nchini humo baada ya awali taifa hilo kuandaa Afcon ya mwaka 1984.

Licha ya Rekodi zetu kutokuwa bora dhidi ya Uganda (kabla ya mchezo wa jana tulikuwa tumekuta na nao mara 59, Uganda imeshinda 32, Tanzania imeshinda 12, na sare 15) lakini bado mchezo wa hapa nyumbani Jumanne ni muhimu na utakuwa wa kwanza kati ya mitatu tulizonazo ili kukamilisha hatua ya makundi, nyingine ni nyumbani dhidi ya Niger na ugenini dhidi ya Algeria.

Kwa kuwa Niger ina alama 2, hii ina maana kwamba tukiitumia vyema michezo yetu dhidi ya Uganda tutakuwa katika nafasi nzuri ya kufanikiwa, hasa kwa kuwa mchezo ujao dhidi ya Niger itacheza tena dhidi ya vinara Algeria, ambao wana nafasi kubwa ya kushinda na ikiwa hivyo itakuwa ni matokeo mazuri kwa Tanzania.

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Pindi Chana alisema serikali itatoa Sh500 milioni kwa Taifa Stars endapo itafuzu ikiwa ni sehemu ya motisha kama ilivyofan ya mara ya mwisho mwaka 2019.

Huu ni mwendelezo wa Serikali chini ya Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kuendelea kutoa motisha baada ya kununua kila bao kwa Shilingi milioni 5 kwenye michuano ya kimataifa kwa timu za Simba SC na Young Africans.

Kiu ya mashabiki ni kuona kikosi hicho kinakuwa na mwendelezo mzuri baada ya kufanya hivyo kule nchini Misri chini ya aliyekuwa Kocha Mkuu Mnigeria, Emmanuel Amunike, ambaye aliiongoza kufuzu kwa mara ya pili kihistoria ikiwa imepita miaka 39 tangu ilipofuzu kwa mara ya kwanza mwaka 1980. Tunawakumbusha wachezaji wetu kupambana hadi mwisho na mashabiki kujitokeza kusapoti.

Shinyanga yakusanya Bilioni 255 shughuli za Madini
Fiston Mayele apeleka salamu TP Mazembe