Washambuliaji wa Simba na Yanga, Laudit Mavugo na Amissi Tambwe hawajajumuishwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Burundi kwa ajili ya michuano ya CECAFA.

Kocha wa timu ya taifa ya Burundi, Alain Olivier Niyungeko ameamua kuingiza damu mpya katika kikosi chake kwa kuteua wachezaji chipukizi wa kikosi cha vijana walio chini ya umri wa miaka 20 pamoja wale wanaocheza ligi ya ndani kwa lengo la kujiandaa na michuano ya kufuzu CHAN mwakani.

Kikosi kamili:

Makipa: Nahimana Jonathan (Vital’O), Nininahazwe Bievenue (Messenger Ngozi), Mutombo Fabien (Lydia Ludic), Rugumandiye Yvan (Musongati), Ndikuriyo Patient (Aigles Noirs),

Mabeki: Ndoriyobija Eric (Lydia Ludic), Suleyman Mustafa (Aigles Noirs), Moussa Omar, Ndizeye Samuel (Athletico Olympic), Nshimirimana David (Vital’O), Nahimana Steve (Aigles Noirs), Kashindi Joseph (Inter Star), Guy Chancel, Harerimana Rashid Leon (Lydia Ludic), Nyandwi Innocent (Magara).

Viungo: Urasenga Cedric Danny (Messenger Ngozi), Rukundo Terence (Aigles Noirs), Ntirwaza Sudi (Musongati FC), Ndikumana Moussa (Athletico Olympic), Nsabumukama Enock (Messenger Ngozi), Ndayishimiye Yousouf (Aigles Noirs), Mbirizi Eric (Bujumbura City), Uwimana Messo (Lydia Ludic), Idi Saidi Djuma, Andre Tokoto (Lydia Ludic), Duhayindavyi Gael (Vital’O).

Washambuliaji: Lomeya Magloire (Olympic Star), Bimenyimana Caleb (Vital’O), Hakizimana Alexis Kitenge (Athletico Olympic), Ndarusanze Jean Claude (Lydia Ludic), Bigirimana Hassan.

Exclusive: Mwanzilishi wa MTV Africa afunguka mpango wa tuzo za MTV kufanyika Dar
TRA yakusanya shil.trilion 1.15 kwa mwezi Oktoba