Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa TAMISEMI imetoa ufafanuzi wa taarifa zinazoendelea mitandaoni kuhusiana na milioni 600 zilizotolewa na serikali katika fedha za msaada kutoka IMF ili kupambana na Uviko 19 za ujenzi wa madarasa hazijulikani zilipo na kusema kuwa, hakuna fedha iliyopotea, Madarasa yameshajengwa kwenye Vituo shikizi.

Aidha Mbarali, Mbeya Kata ya Luhanga ni kati ya kata 20 zilizopo ndani ya Wilaya ya Mbarali Mkoa wa Mbeya na ilipokea Shilingi Milioni 160 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa , ambapo katika vituo shikizi kiasi cha shilingi Mil 470 kutoka mradi wa kuinua ubora wa Elimu ya Sekondari nchini zilipelekwa kwa ajili ya ujenzi wa shule Mpya ya Sekondari.

Hata hivyi ilibainika kuwa Kata hiyo ina mgogoro wa mipaka na hifadhi ya Taifa TANAPA tangu mwaka 2008 ilipotangazwa GN 28 na kuonekana kata hiyo ipo ndani ya Hifadhi, ambapo baadhi ya shughuli za maendeleo zilisitishwa hususan ujenzi wa madarasa hayo kwenye vituo shikizi na shule moja ya Sekondari.

Madarasa ya vituo shikizi yamejengwa katika maeneo ya ambayo hayana mgogoro na shule ya Sekondari bado taratibu za kupata Kata yenye uhitaji unaendelea kwa mujibu wa maelekezo ya ujenzi wa shule hiyo kupitia mradi wa kuinua ubora wa elimu ya sekondari nchini.

Mchanganuo wa wa ujenzi wa Madarasa 8 ya vituo shikizi vilivyokuwa kata ya Luhanga ni Kituo Shikizi Matoka vyumba 2 vya madarasa Kata ya Luhanga kimehamishiwa kituo Shikizi cha Mabambila kata ya Mawindi Kituo Shikizi Mwashota vyumba 4 vya madarasa kata ya Luhanga kimehamishiwa kituo Shikizi cha Muungano 2 Kata ya Utengule Usangu na kituo Shikizi cha kapalambo 2 Kata ya Ipwani Kituo Shikizi Mwika vyumba 2 vya madarasa Kata ya Luhanga kimehamishiwa kituo Shikizi cha Mogelo Kata ya Rujewa.

Nani kuchukua nafasi ya Naibu spika
Mkoa wa Kagera kufunguliwa kimiundombinu