Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) linawatahadharisha watu kutoshika wala kukanyaga nyaya za umeme zilizokatika au kuanguka.

Tahadhari hiyo imetolewa mara baada ya shirika hilo kuanza kufanya ukarabati wa mitambo ya kuzalisha umeme wa kituo cha Ubungo II.

Ukarabati huo unatarajiwa kufanyika kuanzia leo Januari 9, 2019 hadi Februari 13, 2019 kwa kukarabati mitambo ya kuzalisha umeme ukihusisha ubadilishaji wa vipuri ili kuiongezea ufanisi mitambo hiyo.

Kutokana na ukarabati huo baadhi ya maeneo ya Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani pamoja na Zanzibar yataathirika kwa kukosa huduma ya umeme.

Kutokana na usumbufu pamoja na madhara yatayojitokeza Tanesco imeomba radhi kwa umma.

 

Mwanamitindo maarufu auawa siku chache kabla ya harusi yake
Jeshi la Polisi lapiga marufuku maandamano ya Bavicha Serengeti