Nchi wanachama wa Mkataba wa Kimataifa wa Biashara ya Wanyamapori na Mimea iliyo hatarini kutoweka (CITES), imeichagua Tanzania kuwa kuwa mjumbe wa akiba wa Kamati Kuu (Kamati ya Wanyamapori) na mjumbe wa Kamati ya Mimea, kwa kipindi cha miaka mitatu.

Hatua hiyo, imejiri wakati wa mkutano wa 19 wa nchi wanachama wa CITES, uliofanyika nchini Panama ambapo Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Pindi Chana amesema hatua hiyo inatoa nafasi kwa Tanzania kusimamia na kutetea masuala ya kimkakati yenye maslahi kwa uhifadhi na biashara ya kimataifa.

Wajumbe katika mkutano wa nchi wanachama mkataba wa Kimataifa wa Biashara ya Wanyamapori na Mimea iliyo hatarini kutoweka (CITES).

Dkt. Pindi Chana ambaye ameongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo uliohudhuriwa na wajumbe takribani elfu tatu kutoka nchi 153 ambazo ni wanachama wa CITES, amesema biashara hiyo ya kimataifa ni ya mazao ya wanyamapori, misitu na uvuvi na kwamba itasaidia pia kuinua shughuli mbalimbali za jamii na pato la Taifa kwa ujumla.

Aidha, mkutano huo pia umejadili ajenda 89 na mapendekezo 52 ya kuweka, kuondoa au kubadili hadhi ya wanyamapori na mimea katika makundi ya mkataba wa CITES, huku Tanzania ikishiriki kujadili mapendekezo 16 ya kuweka wanyamapori na mimea katika makundi ya mkataba huo.

Rais Samia awatunuku Kamisheni Maafisa JWTZ
Waipinga Serikali uondoaji sheria ya uchochezi