Tanzania imechaguliwa kuwa Mwenyeji wa Mkutano wa Kimataifa wa Utalii wa 65 wa Kanda ya Afrika utakaoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Masuala ya Utalii (UNWTO) kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka 2022 katika Jiji la Arusha huku ukijumuisha Mawaziri wote wa Utalii wa Bara la Afrika.
Katika mkutano huo Tanzania imechaguliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Bajeti na Mipango ya UNWTO kwa kipindi cha muda wa miaka mitatu kuanzia sasa.
Akizungumza nchini Cape Verde katika mkutano huo mbele ya mawaziri 30 wa utalii, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro amewashukuru Mawaziri hao kwa kuipa heshima nchi ya Tanzania huku akiowaomba Mawaziri wote wa utalii kuja kushiriki katika mkutano huo mwakani.