Kwa mujibu wa taarifa zilizotufikia muda huu ni kwamba Mke wa Mwanasiasa Mkongwe Kingunge Ngombale Mwiru, Peras amefariki dunia leo mchana katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa akipatiwa matibabu.

Mkwe wa marehemu ajulikanaye kama Anita katika akaunti yake ya Snapchat ameandika ujumbe usemao “R.I.P mama yangu, asante kwa yote, Mungu akupumzishe mahala pema peponi.”

Uongozi wa Dar24 media unatuma salamu za pole kwa familia ya mwanasiasa mkongwe Kingunge, kama chombo cha habari tutaendelea kuhabarisha kwa kila linalojili na ratiba nzima za mazishi.

Mungu aipumzishe roho ya marehemu kwa amani.

Ashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za utapeli
Mashinji ataja sababu za viongozi kuhama Chadema