Serikali nchini, imesema Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania – TCRA, imeongeza uwekezaji katika teknolojia ya udhibiti wa picha zisizofaa kwa wananchi.
Kauli hiyo imetolewa Bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye wakati akijibu swali la Mbunge wa jimbo Kinondoni, Abbas Tarimba.
Amesema TCRA ipo mbioni kuja na mpango maalum wa kudhibiti picha chafu mtandaoni na kufuatilia wanaozisambaza.
Katika swali lake, Mbunge Tarimba alitaka kujua hatua zinazochukuliwa na serikali katika kudhibiti picha chafu mtandaoni kama ilivyo kwa nchi zilizoendelea.