Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST), imtarifu kutokea kwa tetemeko la ardhi Wilayani Manyoni mpakani mwa Mkoa wa Singida na Dodoma yakiwa na ukubwa wa 4.3 na 4.9 katika kipimo cha Richter.
Tetemeko hilo, linadaiwa kutokea Februari 16, na hii leo ijumaa Februari 17, 2023 kwa nyakati tofauti katika maeneo kadhaa ya mikoa ya Singida ambapo jijini Dodoma hali ya taharuki ilitanda na kusababisha watu waliokuwa kwenye maofisi kukimbilia nje ili kuepuka madhara.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mbali na matetemeko hayo kuzusha taharuki hasa katikati ya jiji la Dodoma na maeneo jirani, hakuna taarifa zozote za madhara zilizoripotiwa kufuatia matetemeko hayo na hata hivyo halikudumu kwa muda mrefu.
Tetemeko husababishwa na nguvu za asili za mgandamizo na miamba kusigana ama kukatika na kupelekea ardhi kutikisika na wakati mwingine huleta madhara ikiwemo vifo na uharibufu wa majengo, miundombinu, mali nk.