Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa ya kupigwa kwa mwandishi wa habari za michezo wa gazeti la Mwanaspoti nchini, Mwanahiba Richard na kiungo wa timu ya Simba SC Mwinyi Kazimoto mjini Shinyanga.

Kufuatia kitendo hicho kilichotokea wakati wa mazoezi, TFF imesema tukio liliofanywa na mchezaji huyo ni kinyume na sheria, taratibu/kanuni zinazoendesha mpira wa miguu nchini, hivyo wanakilaani kitendo hicho kwa nguvu zote.

Kwa kuwa tukio lilitokea wakati wa mazoezi, mpaka sasa TFF bado haijapokea taarifa rasmi kuhusiana na suala hilo.

Hans Poppe Aitamani Dar es salaam Young Africans Iwe Leo Ama Kesho
Aishi Manula Wa Azam FC Alia Na Waamuzi Wa Kibongo