Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), kimesema kuwa kitaendelea na maandalizi ya uchaguzi mkuu wake licha ya Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Harrison Mwakyembe kutishia kukifuta kwa madai ya kujihusisha na mlengo wa kisiasa.

Mvutano huo baina ya TLS na Serikali umekuja zikiwa zimebaki siku  kumi kabla ya chama hicho kufanya uchaguzi huo ambao kwa mara ya kwanza umekuwa na msisimko na vuta ni kuvute kati yake na Serikali.

Dkt. Mwakyembe alisema Serikali haitakubali kuona chama hicho kinajiingiza katika siasa, bali itafuta sheria iliyoianzisha sura ya 307.

Aidha, Rais wa TLS, John Seka amesema kuwa chama hicho hakijajiingiza kwenye siasa na wataendelea na maandalizi ya uchaguzi wao kama kawaida ambao unatarajiwa kufanyika machi 18, mwaka huu.

“Alichokisema Mwakyembe ni kauli ya Serikali lakini sisi tutaendela na maandalizi ya uchaguzi kama kawaida na kama Ilivyopangwa,”amesema Seka.

Hata hivyo, Seka amesema kuwa TLS itaendelea kuzingatia kanuni na miongozo ya kuanzishwa kwake ambapo pia haina mpango wa kuwa chama cha siasa au chama cha kiharakati.

Sebastien Migne Akabidhiwa Jahazi La Congo Brazzaville
Video: Ni ruksa kuikosoa Serikali - Nape, Wateule wa Rais, Wabunge wanavyotunishiana misuli