Kaka wa kiungo kutoka nchini Ujerumani na klabu ya Real Madrid, Toni Kroos, amefichua siri ya ndugu yake kutarajia kucheza soka nchini England msimu wa 2016-17.

Ndugu wa kiungo huyo aitwae Felix Kroos, amefichuia siri hiyo kutokana na fununu kumuandama Toni, kufuatia nafasi yake kwenye kikosi cha Real Madrid kuendelea kuwa shakani siku hadi siku.

Felix ambaye anaitumikia klabu ya Weder Bremen ya nchini kwao Ujerumani, amesema ni kweli ndugu yake ana mipango ya kuondoka nchini Hispania na dhamira iliopo ni kwenda nchini England kusaka changamoto mpya wa soka lake.

Amesema Toni amekua na wakati mgumu wa kudumu katika mfumo wa meneja wa Real Madrid, ambao unaonekana kutoa nafasi kwa zamu dhidi ya viungo wengine kama Luka Modric pamoja na Carlos Henrique José Casimiro.

“Ninadhani hafurahishwi na mpango unaotumiwa na meneja wa Real Madrid na anaamini hakuna njia sahihi ya kuendelea kubaki klabuni hapo zaidi ya kuondoka kabisa nchini Hispania.” Amesema Felix

“Unajua mabadiliko ya benchi la ufundi yamechangia sana suala la Toni, kufikiria kuondoka kwa sababu wakati aliposajiliwa alikuwepo meneja tofauti, ambaye alionyesha kumtumia mara kwa mara, tofauti na ilivyo sasa kwa Zidane.” Aliongeza Felix

“Hata ingelikua mimi ningeliaondoka kwenye klabu kama ya Real Madrid ambayo inashindwa kumtumia mchezaji mzuri kama Toni Kroos, na kusaka mahala pengine pa kucheza kila mwishoni mwa juma.” Alisisitiza ndugu wa mchezaji huyo.

Klabu za Arsenal na Man city zinatajwa kuwa katika mawindo ya kiungo huyo mwenye umri wa miaka 26, ambaye alikuwa sehemu ya kikosi cha timu ya taifa ya Ujerumani kilichotwaa ubingwa wa kombe la dunia kule nchini Brazil mwaka 2014.

Klabu hizo zinatajwa kutokana na Toni Kroos kuvutiwa na mfumo wa uchezaji wake ambao anaamini utamfaa katika changamoto mpya anayoitafuta nje ya Real Madrid.

Jose Mourinho Kumjibu Anaeziba Rizki Yake Man Utd
Ramires Afichua Siri Ya Kuondoka Chelsea