Mwanamuziki Tory Lanez pengine akatupwa jela kwa muda usiopungua miaka 23 ikiwa atakutwa na hatia juu ya kesi inayomkabili ya kumpiga risasi rapa wa kike kutoka nchini Marekani Megan Jovon Ruth maarufu Megan Thee Stallion.

Kwa sasa ni takribani mwaka mmoja, tangu mwanamuziki Tory Lanez kukanusha mashtaka ya kumpiga risasi msanii mwenzie Megan, ambapo Lanez ameamua kuweka mgomo wa kuingia makubaliano na waendesha mashtaka kwenye shauri hilo ambalo anadaiwa kumshambulia kwa kumpiga risasi mbili za mguuni msanii wa kike maarufu Megan Thee Stallion mnamo Julai 2020.

Kwa mujibu wa jarida la Rolling Stone la nchini Marekani, Tory Lanez atahitajika kufika mahakamani kwaajili ya kutoa ushuhuda wa kilichotokea kati yake na Megan usiku wa tukio hilo ifikapo Disemba 14, 2021.

Kulingana na sheria za nchi ya Marekani inaelezwa kuwa kesi ya shambulio la namna hiyo ikiwa Lanez atakutwa na hatia, inawezekana akahukumiwa kutumikia kifungo cha mpaka miaka 23 Jela.

Varane kuikosa Manchester City
Mukoko: Nimepitia changamoto nyingi