Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Geita Gold FC dhidi ya Singida Big Stars FC uliotarajiwa kuchezwa Kesho Jumatano (September 14), umesogezwa mbele mpaka Jumatano ya juma lijalo (September 21).
Mchezo huo ulipangwa kupigwa Uwanja wa Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza, umesogezwa mbele kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Bodi ya Ligi ‘TPLB’.
‘TPLB’ imeelezwa kuwa Mchezo huo umesogezwa mbele ili kuipa nafasi timu ya Geita Gold FC kusafiri na kupumnzika kuelekea Mchezo wa Marudiano wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika hatua ya awali, ambapo Klabu hiyo itacheza dhidi ya Hilal Al Sahil ya Sudan.
Mchezo Kati ya Geita Gold dhidi ya Hilal Al Sahil utachezwa Jumamosi (September 17), kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi jijini Dar es salaam.
Mchezo wa Mkondo wa kwanza uliopigwa mjini Omdurman-Sudan Jumapili (Septemba 11), Geita Gold FC 0ilikubali kupoteza kwa 1-0.
Tayari Klabu ya Singida Big Stars imeshathibitisha kupokea taarifa ya Bosi ya Ligi na imesisitiza kuwa tayari kukipiga na wenyeji wao Septemba 21, ugenini jijini Mwanza.