Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetoa mafunzo ya siku moja kwa madalali wa Bima Tanzania yenye lengo la kuwajengea uwezo wa kuifahamu  vema Sheria ya Kodi ya Mwaka 2014 ili waweze kushiriki vema kuondoa kasoro katika ulipaji kodi ya ongezeko la thamani kutoka sekta ya bima.

Mafunzo hayo yametolewa na Meneja wa Elimu ya Mlipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Diana Masalla wakati wa mkutano na waandishi wa habari kwenye semina ya siku moja kwa madalali hao ya kuwajengea uwezo kuhusu Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT).

Aidha amesema kuwa mafunzo hayo yamewaelimisha wanachama hao juu ya kodi ya zuio, utoaji wa kodi ya Thamani(VAT) na jinsi ya kulipa kodi kwa njia ya mtandao.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha madalali Tanzania, Mohamed Jaffer ameipongeza TRA kwa hatua yake ya kutoa Elimu kwa wanachama wake kwani imesaidia  sana kuwajengea uwezo amabao utasaidia ulipaji wa kodi hizo.

Polisi wazuiwa kuwavisha mabango madereva wanaokiuka sheria barabarani
Ridhiwani awapongeza watendaji Chalinze