Marekani kupitia hotuba ya Rais, Donald Trump amesikika akiwashutumu wahamiaji wanaoingia nchini humo kwa kutoa maneno yaliyotafsiriwa kama matusi kwa mataifa hayo lengwa.

Trump akiwa katika ofisi yake ndani ya Ikulu ya Whitehouse, ametoa tamko ambalo linawadhalilisha watu kutoka Afrika, Haiti na El Salvator akidai kuwa watu wa matifa hayo ni wachafu hivyo anahoji kwa nini Marekani inawaruhusu kuingia nchini mwao.

Ambapo vyombo mbalimbali vya habari vimethibitisha tamko hilo la Trump ambapo Gazeti la The Washington Post, limeyanukuu maneno ya Rais Trump pindi alipokua akiongea na Wabunge Ikulu Whitehouse.

”Kwa nini tunawaruhusu watu hawa kutoka mataifa ‘machafu”?.Amehoji Trump.

Hata hivyo msemaji wa Ikulu ya Marekani amesema Wanasiasa wa Washington wanapenda kupigania mataifa ya kigeni, lakini rais Trump atawapigania raia wa Marekani pekee.

 

TLS yaeleza mamilioni yaliyokusanywa gharama za matibabu Lissu
Tatizo la rushwa ya ngono vyuoni kushughulikiwa vikali