Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk Ashatu Kijaji amesema wizara yake imeanza kuchukua hatua kali za kisheria kwa watumishi wa taasisi za elimu ya juu (vyuoni) wanaotumia wadhifa wao kuomba rushwa ya  ngono  kwa wanafunzi na kisha kuwapa alama za juu za ufaulu tofauti na uwezo wao kitaaluma.

Kijaji ametoa angalizo hilo jijini Arusha alipokua akizungumza na watumishi wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa chuo cha Uhasibu cha Arusha.

Akizungumza kwa niaba ya watumishi hao makamu Mwenyekiti wa Baraza la wafanyakazi Juma Kaniki ameahidi kuhakikisha maadili yanasimamiwa huku akitumia fursa hiyo kuiomba serikali kuongeza idadi ya watumishi.

Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqaro aliyeambatana na Naibu Waziri amewakumbusha wajumbe wa Baraza la wafanyakazi kuepuka kuwa chanzo cha migogoro ndani ya taasisi.

Ushauri kwa wanafunzi wa vyuoni, wapunguze au waache kabisa starehe zinazowafnya kushindwa kuhudhuria vipindi na kujikuta wanaingia katika mitego ya kushiriki ngono na wakufunzi wao ili wapate alama za juu.

Trump akerwa na Waafrika, awatolea lugha chafu
Wanawake wapigwa marufuku kunywa pombe kwa miaka 60