Rais wa Marekani, Donald Trump amelaani vikali kitabu maarufu kilichochapishwa kilichojaa ukosoaji wa hali ya juu wa mwenendo wa maisha yake ya kisiasa tangu nyakati za kampeni ya uchaguzi.
Trump amesema kuwa kitabu hicho kinachoitwa ‘Fire and Fury: Inside the Trump White House’ kikiandikwa na Michael Wolff kimejaa uongo wa kutupwa.
Kitabu hicho kilichofanya mahojiano na mamia ya watu, kimeeleza kuwa mkutano wa mtoto wa Trump na kundi la maafisa wa Urusi ni uhaini kwa Marekani.
Wanasheria wa Trump wamekuwa wakijaribu kuzuia uchapishwaji wa kitabu hicho bila mafanikio, na sasa kinaingia sokoni.
Kutokana na mambo ya ndani ya kifamilia na Ikulu ya Marekani yaliyoainishwa ndani ya kitabu hicho, kimekumbana na ukosoaji wa hali ya juu.