Marekani imepitisha vikwazo vipya vya zuio la kuingia nchini humo huku Korea Kaskazini ikiingia kwenye orodha ya nchi ambazo raia wake hawaruhusiwi kuingia katika taifa hilo.

Tangu kuingia kwa rais Tramp katika Ikulu ya Whitehouse amekuwa na msimamo wa kuweka zuio la baadhi ya mataifa kuingia Marekani na mataifa mengine yaliyoingizwa katika vikwazo hivyo ni Venezuela na Chad.

Wakati Korea Kaskazini, Venezuela na Chad zikiwekewa zuio la kuingia Marekani nchi ya Sudan imeondolewa katika nchi sita za kiisamu ambazo Rais Trump alikuwa ameziwekea vikwazo.

Sababu zilizopelekea Marekani kuweka vikwazo kwa raia wa nchi hizo kuingia nchini humo ni pamoja na usalama wa nchi zao kuwa duni na ukosefu wa ushirikiano.

Hatua hiyo ya Marekani imetoa masharti tofauti kati ya nchi na nchi ambapo kwa nchi ya Venezuelawale waliozuiwa kuingia Marekani ni wafanyakazi wa serikali na familia zao.

Mataifa mengine ambayo yaliopigwa marufuku na Donald Trump kuingia Marekani ni pamoja na Iran,Libya,Somalia na Yemen.

 

 

Video: Mapya ya Lissu, Rais aamuru mwanawe auawe
Magazeti ya Tanzania leo Septemba 25, 2017