Iran imeipuuzia hotuba ya kwanza ya Rais wa Marekani, Donald Trump aliyoitoa katika Baraza la Umoja wa Mataifa Jijini New York na kuiita kuwa ni hotuba ya kichochezi na iliyojaa chuki dhidi ya nchi hiyo.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Iran, Mohammad Javad Zarif katika mtandao wake wa Twitter ambapo ameiita hotuba hiyo ya Rais Trump kuwa ni ya zama za kale.

Aidha, Rais wa Marekani katika hotuba yake hiyo ameituhumu serikali ya Iran kwamba ina utawala wa kidikteta na wa kifisadi hivyo amependekeza kuwa hatayaheshimu makubaliano ya nyuklia yaliyofikiwa chini ya uongozi wa Rais wa zamani wa nchi hiyo Barack Obama.

Vile vile Rais Trump katika hotuba yake hiyo ametishia kuiteketeza Korea kaskazini iwapo itaendelea na shughuli zake za kinyuklia ambazo zinahatarisha usalama wa Marekani na washirika wake.

Hata hivyo, Rais huyo wa Marekani katika hotuba yake hiyo ya Baraza la Umoja wa Mataifa pia ameionya nchi ya Venezuela kwa kuitaka kumaliza mgogoro wa kisiasa ulioikumba nchi hiyo huku akisema kuwa atamshughulikia Rais wa nchi hiyo, Nicolas Maduro.

 

Burundi yataka wapenzi kuoana kilazima, yatoa muda
Serikali yatoa onyo kali kwa watumiaji wa barabara