Serikali ya Burundi imewaamuru wananchi wake ambao ni wapenzi kuhalalisha mahusiano yao kwa kuoana kabla ya kuisha kwa mwaka huu 2017, ikiwa ni njia mojawapo ya kukuza maadili nchini humo.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Terence Ntahiraja amesema kuwa miaka ya karibuni kumekuwa na ongezeko la watu pamoja na mimba za mashuleni hivyo lazima jitihada zichukuliwe kukabiliana na changamoto hiyo.

Kufuatiwa agizo hilo, Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza ametangaza kuanzisha kampeni ya kuhamasisha jamii kukuza maadili katika nchi ambayo miaka miwili iliyopita ilikua katika ugomvi mkali wa kisiasa.

Aidha Ntahiraja amefunguka kuwa nchi inakumbwa na tatizo la ongezeko kubwa la watu kutokana na ndoa zisizo za uhalali amesema kuwa ongezeko hilo ni kutokana na mwananume mmoja kumiliki wake wengi pia  wasicahana wengi waliopo mashuleni kushika mimba zisizotarajiwa.

Hivyo amesema kuwa makanisa na serikali ndio suluhisho la tatizo hilo, amewakumbusha kuwa ni jukumu lao kuhakikisha jamiii inakuwa katika njia iliyosawa.

”Waburundi wanatakiwa kuwa na upendo baina yao na nchi yao, upendo huo unaoneshwa kwa kuoana” Amesema Ntahiraja.

Gavana wa kusini-mashariki  katika mji wa Rutana ameamuru kuwa wanaoishi katika vyama vya umoja wa sheria ‘wanapaswa kuwekwa kwenye orodha maalumu mnamo Juni 22, wakati Gavana wa jimbo la Kaskazini–magharibi Bubanza ametaka kuwepo kwa vikawazo visivyojulikana dhidi ya wakiukaji wa agizo hilo.

 

 

Liverpool yatupwa nje michuano ya Carabao
Trump azionya Iran, Korea Kaskazini na Venezuela