Rais wa Marekani, Donald Trump na mwenzake wa Urusi, Vladimir Putin wamekubaliana kuhakikisha wanaliangamiza kundi la wapiganaji wanaojiita Islamic State (IS) na kutoa msaada kwa wanajeshi wa Syria ili kuweza kulitokomeza kundi hilo.
Ikulu ya Urusi imesema kuwa marais hao walikutana faragha pembezoni mwa mkutano wa viongozi wa Asia na Pasific unaofanyika nchini Vietnam na kujadili kuhusu kundi hilo kuliangamiza.
Aidha, Ikulu ya White House haijasema chochote kuhusu mkutano wa wawili hao, ingawa taarifa zinasema kuwa wamekubaliana kwa pamoja kuliangamiza kundi la Islamic State ambalo limekuwa likisababisha vifo vya watu wasiokuwa na hatia.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Interfax la Urusi, limesema kuwa wameahidi kuendelea kudumisha njia za mawasiliano za kijeshi kati ya majeshi ya Urusi na Marekani ili kuzuia uwezekano wa kushambuliana wakati wakishambulia IS