Nahodha msaidizi wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ amesema kushinda mchezo wa kesho Jumapili (Julai 25), ndio kutaleta taswira ya ukubwa wa klabu hiyo.

akizungumza na waandishi wa habari dimbani Lake Tanganyika mkoani Kigoma ‘Tshabalala’ amesema kuna umuhimu kwa kila mchezaji wa Simba SC kupambana hadi tone la mwisho, ili kudhihirusha kuna kitu wanakihitaji.

Amesema Simba SC ni klabu kubwa yenye mashabiki wenye kiu ya ubingwa hasa unapofika mchezo wa Fainali kama wa kesho Jumapili (Julai 25).

“Kufanya vizuri kesho ndio italeta taswira ya ukubwa wa Simba SC.” Amesema ‘Tshabalala’

Simba SC inayoshikilia ubingwa wa ASFC, itapambana dhidi ya Young Africans kesho Jumapili (Julai 25), Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma.

TTCL yatakiwa kuonesha ushindani
Gomes: Nina deni kubwa Simba SC