Kocha wa Klabu Bingwa Tanzania Bara Simba SC, Didier Gomes, amesema kikosi chake kipo tayari kuikabili Young Africans kwenye mchezo wa Fainali Kombe la Shirikisho kesho Jumapili (Julai 25).

Gomes ameeleza utayari wa kikosi chake alipozungumza na waandishi wa habari mkoani Kigoma leo Jumamosi (Julai 24).

Kocha huyo kutoka nchini Ufaransa amesema malengo makubwa ya Simba SC ni kushinda mchezo huo ili kuwapa furaha mashabiki na wanachama wao.

Amesema anafahamu ana deni la kutetea taji la Kombe la Shirikisho (ASFC), baada ya kufanya hivyo kwenye Ligi Kuu kwa kutetea ubingwa kwa mara ya nne mfululizo.

“Tunataka kumaliza msimu huu vizuri, tunataka mashabiki wetu wajisikie vizuri”

“Tunajua mchezo utakua mgumu, lakini tumejiandaa kukabiliana na Young Africans kwa hali yoyote ile, ili tufikie lengo la kupata ushindi.

Mchezo wa Fainali Kombe la Shirikisho utaanza majira ya saa kumi jioni, Uwanja wa Lake Tanganyika.

'Tshabalala': Kuna umuhimu wa kila mchezaji kupambana hadi mwisho
Young Africans watembelea Subira Mina Rahman