Viongozi, Benchi la Ufundi, Wachezaji, Wakiongozwa na Mwenyekiti wa Young Africans Dkt. Mshindo Msolla leo Jumamosi (Julai 24), wametembelea kituo cha watoto yatima cha Subira Mina Rahman kilichopo Kigoma Mjini.

Young Africans walifika kituoni hapo majira ya asubuhi na kuzungumza na viongozi wa kituo hicho, na kisha kutoa sehemu ya mahitaji.

Huu umekuwa ni utamaduni wa klabu hiyo kongwe katika Ukanda wa Afrika Mshariki na Kati ikiwa ni sehemu ya kurudisha kwa jamii.

Mbali na hatua ya kurudisha kwa jamii, Young Africans pia wanakusudia kufanya kilicho bora ili kuleta furaha kwenye maisha ya kila mtu anayehusika na klabu hiyo.

Kikosi cha Young Africans kipo mkoani Kigoma kwa ajili ya mchezo wa Fainali Kombe la Shirikisho (ASFC), dhidi ya Simba SC.

Mchezo huo utachezwa kesho Jumapili (Julai 25), majira ya saa kumi jioni Uwanja wa Lake Tanganyika.

Gomes: Nina deni kubwa Simba SC
Mangungu: Yaacheni ya Haji Manara na Barbara