Mwenyekiti wa Tume ya haki za binadamu na utawala bora, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu amesema wameanza uchunguzi ili kubaini ukweli kuhusu taarifa zinazozagaa mtandaoni zikihusisha ajali ya Naibu waziri wa Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali Za Mitaa – TAMISEMI, Dkt. Festo Ndugange.

Akizungumza na Waandishi wa habari hii leo Mei 10, 2023 Jijini Dodoma, Jaji Mstaafu Mwaimu amesema hatua hiyo inatokana na uwepo wa taarifa za vyombo vya habari zenye mkanganyiko hasa mitandao ya kijamii, kuhusu ajali hiyo kuhusishwa na kifo cha Mwanafunzi wa Chuo kikuu cha Dodoma -UDOM, Nusura Abdallah.

Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala  Bora Jaji Mstaafu, Mathew Mwaimu.

Amesema, “tume ya haki za Binadamu na utawala bora inatambua kuhusu kuwepo kwa vyombo vinavyoshughulikia masuala ya haki Jinai hususan Jeshi la polisi, kunapotokea Mashaka kutoka kwa Wananchi kuhusu jambo lolote linaloashiria uvunjwaji wa haki za binadamu au mashaka ya haki kutotendeka.”

Mwenyekiti huyo ameongeza kuwa, “tume inamamlaka ya kufanya uchunguzi juu ya jambo hilo kwa mujibu wa katiba na sheria ya tume kwa kuwa inajukumu la kutetea na kulinda haki za binadamu Nchinim kwa mujibu wa kifungi cha 15 (1) cha sheria ya tume ya haki za binadamu na utawala bora sura ya 391 na tume inayo mamlaka ya kuanzisha uchunguzi.”

Ahmed Ally: Sijui watakaosajiliwa Simba SC
Juventus kurudisha dimba Mason Greenwood