Siku chache zilizopita Hit maker wa Niroge Vanesa Mdee ‘Vee Money’ alisema wameamua kutokuanika mahusiano yake yeye pamoja na msanii mwenzake Juma Jux kutokana na kuwa wanahitaji kuwa na usiri katika maisha yao binafsi.

Vanesa pamoja na Jux mahusiano yao yalianza takribani mwaka na nusu uliopita ambapo mwanzo wawili hao walikuwa wakikataa kuweka uwazi mpaka pale walipoamua wao kuweka wazi kuonesha kuzidiwa na na penzi.

Jux alikaririwa mwaka jana katika kipindi cha ala za roho cha Clouds fm kwamba Vanesa akiwa tayari muda wowote yupo tayari kumvisha pete akionesha jinsi gani haoni na hasikii kwa mtoto huyo wa kipare hali iliyozidi kuwapa furaha mashabiki zao kwa kuona jinsi  gani wasanii hao wanapendana.

Baada ya wao kuamua kutosambaza tena picha zao wakiwa wawili watu wengi walianza kuhisi kwamba mambo yamekwenda kombo na kuwa wapenzi hao wameachana kitu ambacho kwa upande wao wamekanusha na kusema wameamua kuishi maisha ya usiri (privacy life)

“Tumefika kipindi ambacho tuyaweke mahusiano yetu privacy na mziki wetu uendele, bado mimi na Vanessa Mdee ni wapenzi”-jux.

Jana katika kipindi cha xxl cha Clouds fm wakati akitambulisha wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la wivu Jux amewataka mashabiki wao waendelee kusapoti kazi zao ili zifike mbali zaidi.

TFF Yaichinjia Baharini Stand Utd Kampuni
Necta Yatoa Pongezi kwa Kamati ya Usimamizi wa Mitihani ya Ualimu, Mmoja afutiwa Matokeo