Baraza la mitihani Necta limetoa pongezi kwa kamati za uendeshaji mitihani ngazi za mikoa mpakawasimamizi nchini kwa kuzingatia taratibu za uendeshaji mitihani nchili iliyofanyika Mei 2016.

Pongezi hizo zimetolewa leo na Katibu Mtendaji NECTA Dkt Charles Msonde leo wakati akitoa taarifa za matokeo ya ualimu wa ngazi ya cheti pamoja na stashada na kusema usimamizi thabiti ndio uliofanya urahisi wa matokeo kupatikana.

Akitangaza matokeo ya Ualimu leo kwa wanahabari Dkt Msonde amesema kuwa ngazi ya cheti jumla ya waliofanya mitihani ni 10,887 waliofaulu ni 10747 watakaorudia ni wawili huku walioshindwa mitihani ni 18 na kwa ngazi ya stashada ni kati ya watahiniwa 415 waliofaulu ni 337 na watakaorudia ni 49 huku walioshindwa mitihani ni 13.

Aidha katika watahiniwa hao waliofanya mitihani ya kuhitimu Mei mwaka huu mtahiniwa mmoja wa ngazi ya cheti amefutiwa matokeo yake kwa udanganyifu alioufanya wakati wa mitihani.

Dkt Msonde amesesisitiza pia wafanyakazi pamoja na wanafunzi wanaotumia vyeti vya kughushi mitaani wajisalimishe kwa kuacha mara moja kabla ya kukamatwa kwa msako ambao bado unaendelea kwa kua vyeti halali vitokavyo Baraza vina utofauti mkubwa ndio maana wengine wameweza kukamatwa pamoja na kutumia nembo yao (Necta)

Hata hivo matokeo yote ya mitihani ya ualimu yanapatikana katika tovuti za baraza la mitihani kama www.necta.go.tz  auu www.tanzania.go.tz

Tumeamua Tuyaweke Mahusiano Yetu Privacy- Jux
Video: Matokea Kidato cha Sita 2016 Yatangazwa