Jeshi la Polisi Wilaya ya Hanang’ Mkoa wa Manyara, limewataka Wananchi kutumia vikundi vya ulinzi shirikishi vilivyopo, ili kuzuia na kutanzua uhalifu katika jamii.

Kauli hiyo, imetolewa na Mkuu wa Polisi Wilayani humo Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, SSP. Amina Kahando wakati akitoa elimu ya miradi wa Polisi, ikiwemo ushirikishwaji wa jamii.

Amesema, katika kuhakikisha dhana ya usalama wa raia na mali zao inatekelezwa kwa vitendo, pia Wazazi hawana budi kufuatilia mienendo ya vijana wao ili kuwaepusha kujiingiza kwenye kutenda uhalifu.

Hata hivyo, Jeshi la Polisi Wilaya ya Hanang’ limekuwa likitoa elimu ya Miradi mbalimbali ya Polisi, likilenga kuongeza ushirikishwaji wa Jamii katika kulinda raia na Mali zao.

Mbappe arudisha imani kwa mashabiki
Gamondi awaonya Maxi, Aziz Ki, Mkude