Sheria ya Tanzania inatambua kosa la ubakaji kupitia kifungu 130 cha makosa ya jinai ambapo imeeleza mtu atakaye muingilia binti, msichana au mwanamke kinguvu kwa kutumia ushawishi, mazingira mengine ama akubali kwa ridhaa yake iliyopatikana kwa njia ya udanganyifu, atakuwa amefanya kosa la kubaka.
Hayo yamebainishwa na Wakili wa kujitegemea, Yasini Hassan wakati akizungumza na Dar24 Media na kusema kifungu cha 130 kimetamka moja kwa moja kuwa mtu anayeweza kumuingilia mwanamke ni mwanaume, na ilianza kuwa kwenye kifungu cha 129 ikieleza kwa tafsiri ya kifungu hiki cha 130 ikimjumuisha mtu mzima na msichana.
Amesema, “mtendaji kwenye kosa hili ni mwananume na ndio kosa ambalo limewekea jenda kwamaana mjinsia ya mtendaji kwenye hili kosa ni mwananume mwanaume kumuingia mwananmke au msichana kinguvu pasipo kupata ridhaa yake ama amepata ridhaa yake kwa njia ya udanganyifu atakuwa ametenda kosa la kubaka Mwanamke hana nafasi ya kuwa ametanda kosa la kubaka.”
Na alipoulizwa endapo mwanamke atamlazimisha mwanaume kufanya tendo sheria inasemaje, Yassin alisema “sheria imemtamka mwanaume akiwa amelazimisha kutenda tendo kwa mujibu wa sheria yetu hii kuanzia kifungu cha 129 ikitamka kabisa inavyosema mwananmke ni nani manaake imetoa mwanamke ndio mtendewa.”
Aidha, amesema kwa mujibu wa sheria mwanamke hana nafasi ya kuonekana ametenda kosa la kubaka na kwa tafsiri ya sheria ina mazingira yake ambayo inaonesha ni namna gani unaweza ukasema tendo la kubaka limetokea yakimtaja mwanaume na si mwanamke kwani yeyote kati ya wawili hao akifanya atakuwa ametenda kosa la kubaka.