Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Mkonda leo amemuapisha Mkuu mpya wa Wilaya ya Ubungo aliyeteuliwa hivi karibuni na Rais John Magufuli.

Mkuu huyo wa wilaya Bw. Humphrey Polepole ameapishwa leo julai 11 kukamilisha idadi ya wakuu wa tano wa Dar es salaam, wenzake wanne waliapishwa wiki iliyopita wakati yeye akiwa kwenye matatizo ya kufiwa na Baba yake mzazi

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amemuapisha Mkuu huyo wa wilaya ya ubungo kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa Ilala Dar.

Hata hivyo Mh. Polepole amesema wataziondoa kero zote za wana ubungo pia kujiandaa kuweka ofisi ya Wilaya na itakapokamilika wananchi watapewa taarifa kwa kushirikiana na Mkoa ,na kutekeleza yote waliyokuwa wamekubaliana kwenye ngazi za Wilaya.

Kupitia ukurasa wake wa twita Mh. Polepole  amewataka wananchi wa ubungo kushirikiana na ili kutengeneza wilaya ya tofauti.

”Hodi Ubungo, mh. Rais amenituma niwe mtumishi na kiongozi kwenu. Ubungo tutakuwa Wilaya ya Tofauti. Tushirikiane”. ameandika Polepole

 

Tanzania Yathibitisha Ushiriki Wa Beach Soccer
Video: Highlights za Finali na Matukio Yaliyovutia EURO 2016