Mahakama ya juu nchini Kenya itatoa uamuzi wa muda wa mwisho kuamua iwapo marudio ya uchaguzi wa urais yanaweza kufanyika siku ya Alhamisi au kuahirishwa tena kama ilivyokuwa hapo awali.
Mahakama hiyo itasikiliza ombi la dharura siku ya Jumatano kuhakikisha kuwa uchaguzi huo unafutwa ama kuahirishwa kufanyika mpaka pale kasoro zinazolalamikiwa na muungano wa vyama vya upinzani NASA zitakaporekebishwa.
Aidha,Mahakama ya juu nchini humo imekubali kusikiliza ombi hilo la muda wa lala salama ambalo linahoji iwapo tume ya uchaguzi na mwenyekiti wake wataweza kufanya uchaguzi ulio huru na haki siku ya Alhamisi.
Hata hivyo, kwa upande wake Rais wa sasa wa nchi hiyo, Uhuru Kenyatta amesema kuwa uchaguzi huo ni lazima ufanye huku akiwa na muswada wa uchaguzi katika meza yake unaotarajiwa kutiwa saini muda wowote.