Imeandikwa na Charles Abel (@charlesabel24)

Kwenye ‘Derby’ jana Jumamosi (Julai 03) kulitokea tukio la mwamuzi msaidizi namba 1 kuingia ndani ya uwanja wakati Simba wakishambulia.

Wengi Tumepigwa na mshangao kwa sababu ni Tukio jipya kuliona.. LAKINI Kwa Taratibu za CAF na FIFA, mwamuzi msaidizi, FRANK KOMBA ALIKUWA SAHIHI.

Kivipi? Unaweza ukawa unajiuliza hivi.

Kwa kawaida kwenye mchezo mwamuzi wa kati anatakiwa kuwa karibu na mpira (umbali wa Yadi 10) na pia kuwa kwenye angle nzuri ya kuona Tukio.

Kwenye Kaunta Attack [Kama hili shambulizi la Simba] Mwamuzi wa kati alikuwa mbali na hakuna namna angeweza kuliona hili tukio kwa angle nzuri zaidi

Hapa ndipo Mwamuzi wa msaidizi atakapotakiwa kuswitch kutoka Law 11 [OFFSIDE] na kwenda kwenye Law 12 [Fouls ans Misconduct]

Mwamuzi wa msaidizi atatakiwa kusogea karibu na tukio kuangalia kama kuna madhambi yatatendeka, Yatatendeka eneo lipi na kwa ukubwa upi.

Hivyo kwa Tukio la Jana, Mwamuzi msaidizi namba 1 FRANK KOMBA ALIKUWA SAHIHI SANA.

Na hii ndio Faida ya uzoefu anaoupata kwa kuchezesha michezo mikubwa ya CAF

Ikumbukwe Komba ni miongoni mwa waamuzi waliochezesha mchezo wa Robo Fainali, Kombe la Shirikisho CAF kati ya Orlando Pirates dhidi ya Raja Casablaca

Hongera sana @kombafrank

Vurugu yaibuka timu ya taifa ya Ufaransa
Zulu afaulu vipimo Azam FC