Hali si shwari kwenye kikosi cha Ufaransa baada ya kutupwa nje ya michuano ya UEFA Euro 2020, kufuatia malumbano yanayodaiwa kuibuka ndani ya kikosi hicho.

Imeelezwa kwamba wachezaji wa kikosi hicho, Kylian Mbappe ambaye alikosa mkwaju wa penati na kuiponza timu hiyo kutupwa nje ya michuano, ameingia kwenye malumbano na Antoine Griezmann.

Wengine waliodaiwa kuwa kwenye malumbano ni viungo wawili, Adrien Rabiot na Paul Pogba kwenye vyumba vya kubadilishia nguo, kabla ya malumbano mengine kuonekana hadharani wakati wazazi wa wachezaji hao kuonekana kulumbana jukwaani walipokuwa wakiwatazama watoto wao wakiwajibika uwanjani.

Kinachoelezwa ni kwamba Mbappe, amekuwa na wivu juu ya umaarufu wa Griezmann kwenye kikosi cha Ufaransa, ambacho kitajipanga upya ili kutetea taji la Dunia mwaka 2022.

Mbappe anahesabika kama mmoja wa mastaa maarufu duniani, lakini habari ni tofauti linapokuja suala la kuitumikia Ufaransa, Griezmann amekuwa kipenzi cha mashabiki kwenye timu hiyo.

Mbappe aliwahi kutibuana pia na Olivier Giroud.

Waziri Aweso: Sishindwi kuwachukulia hatua
Ufafanuzi mwamuzi msaidizi kuingia uwanjani