Muungano wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Nchini Uganda umekataa agizo alilolitoa Rais wa Uganda Yoweri Musevi la  Vyombo vyote vya Habari kurusha hotuba yake kila Jumapili saa moja hadi saa tatu usiku

Muungano huo umesema katika msimu wa kampeni hawawezi kutoa fursa kwa mgombea mmoja pekee bila kuzingatia wagombea wengine.

Kulingana na Sheria ya Utangazaji ya Uganda ya mwaka 2013, kila mgombea anastahili kupewa nafasi sawa katika Vipindi na Habari zinazochapishwa au kupeperushwa na Vyombo vyote vya Habari nchini humo.

Msemaji wa Museveni, Don Wanyama, alitangaza kuahirishwa kwa hotuba hiyo baada ya Vyombo vya Habari kukataa kurusha hotuba hiyo.

Tanzania yaithibitishia Jumuiya ya kimataifa kuendelea kulinda amani
Jela miaka miwili kwa kuisababishia hasara TCRA

Comments

comments