Ujerumani inaadhimisha kumbukumbu ya miaka 80 tangu kuzuka kwa ghasia kubwa zilizofanywa na wafuasi wa Nazi dhidi ya Wayahudi. yaliyopelekea Wayahudi 100 kuuawa katika machafuko hayo yaliyoripuka Novemba 9 hadi 13, 1938.
Rais wa Shirikisho la Ujerumani, Frank Walters-Steinmeier na Kansela Angela Merkel wataungana pamoja na wajumbe wa Baraza Kuu la Wayahudi nchini Ujerumani hii leo kwenye kumbukumbu ya miaka 80 tangu kuzuka kwa ghasia kubwa zilizofanywa na wafuasi wa Nazi dhidi ya Wayahudi.
Katika ghasia hizo, mamia ya masinagogi na biashara zilizokuwa zikimilikiwa na Wayahudi ziliharibiwa na kuchomwa moto, huku mamia kwa maelfu ya Wayahudi wakidhalilishwa hadharani na kufukuzwa nchi. ambapo inadhaniwa kuwa takribani Wayahudi 100 waliuawa katika machafuko hayo.
Aidha, kuzinduliwa kwa kampeni hiyo ya uhalifu uliofanywa na utawala wa Kinazi dhidi ya Wayahudi walioishi Ujerumani, baadaye kulitambulika kama usiku wa Kioo Kilichovunjika, kwa kuwa mitaa yote ilifunikwa na vifusi vya vioo vya madirisha ya mali zilizomilikiwa na Wayahudi, ambayo yaliharibiwa vibaya.
-
Marais wanne wa zamani wachuana tena Madagascar
-
Ikulu ya Marekani yafuta kibali cha mwandishi aliyejibizana na Trump
-
Mwanasheria mkuu wa Marekani ajiuzulu
Hata hivyo, Rais wa Baraza la Wayahudi, Josef Schuster pamoja na Kansela Merkel wanatarajiwa kutoa hotuba katika Sinagogi lililopo kwenye mtaa wa Ryke mjini Berlin, ambapo zitarushwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha umma. huku wageni mbalimbali maarufu kutoka kada za kisiasa, sayansi, viwanda, kanisa na tamaduni, pia watahudhuria.