Wabunge wa vyama vya upinzani vinavyounda Ukawa wameonywa kutofanya jambo lolote litakaloashiria kuvuruga Bunge wakati Rais John Magufuli atakapolihutubia leo jioni.

Akiongea jana mjini Dodoma, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mtama, Nape Nnauye alisema kuwa Wabunge hao wa Ukawa wanapaswa kufahamu kuwa kitendo chochote watakachofanya kwa lengo la kuvuruga hotuba hiyo ni kinyume cha sheria na taratibu za Bunge na kwamba hawatavumiliwa.

nape (1)

Nape alionesha kuwashangaa wabunge hao kudai kuwa hawamtambui Rais Magufuli ili hali wanashiriki katika shughuli zote za Bunge ikiwa ni pamoja na kumpigia kura Waziri Mkuu ambaye ameteuliwa na Rais huyohuyo wanaedai hawamtambui.

Naye Mbunge wa jimbo la Nzega, Dkt Khamis Kigwangala alisema kuwa wabunge wa Ukawa wana haki ya kuingia Bungeni na kukaa kwa utulivu au kutoka nje endapo hawatakuwa tayari kusikiliza hotuba hiyo lakini sio kuvuruga hali ya amani ili watanzania wasipate nafasi ya kumsikiliza Rais.

“Hawawezi kuwanyima haki watanzania kumsikiliza Rais wetu akiwa anatoa dira ya uelekeo wa Taifa letu,” alisema Khamis Kingwangala.

Wabunge wa Ukawa jana walifanya mkutano na vyombo vya habari na kueleza kuwa hawatakubali kumuona Rais wa Zanzibar, Dkt Ali Mohamed Shein akiingia katika Bunge hilo leo kwa kuwa kipindi chake cha urais Zanzibar kimekwisha. Walisisisitiza kuwa watafanya ‘jambo’ ambalo hata hivyo hawakulitaja. Wabunge hao pia walisema kuwa wamemuandikiabarua Spika wa Bunge kuhoji uhalali wa hotuba ya Rais wakati Zanzibar bado haijampata Rais mpya.

 

Dkt Shein ashauriwa kutohudhuria Bungeni leo
Arsene Wenger Amalizana Na Sanchez, Ozil