Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amesema kuwa endapo Tume ya Uchaguzi na Serikali haitasogeza mbele uchaguzi mdogo wa Wabunge unaotarajiwa kufanyika Januari 13, 2018 basi UKAWA hawatashiriki uchaguzi huo.
Amesema kuwa Tume ya Uchaguzi inapaswa kuahirisha uchaguzi huo kwanza ili ifanyike tathmini na wadau wa siasa waweze kuzungumza mambo mbalimbali ambayo wamejifunza kupitia uchaguzi mdogo wa udiwani.
Aidha, ameongeza kuwa endapo Serikali na Tume ya Uchaguzi haitaiona umuhimu wa kuahirisha uchaguzi huo basi wao kama UKAWA hawatashiriki uchaguzi huo.
“Kuendelea kushiriki chaguzi za kuumiza watu, kufunga watu, chaguzi za kuvunja amani hazitujengi kama taifa bali tunaongeza mpasuko na ufa kati yetu, hivyo sisi rai yetu uchaguzi huu usogezwe mbele wadau tukae kwanza, vyama vya siasa tuzungumze,”amesema Mbowe