Ama kweli! jambo huzua jambo na ndio maana Wahenga walikuwa wakitoa misemo mingi ambayo ilitokana na uhalisia wa tukio au jambo lenyewe.

Na moja kati ya msemo wa wahenga ambao unarandana na Habari yetu ya leo ni ule wa “Ukitaka uzuri sharti udhurike,” sina hakika hapa walikusudia nini lakini kuna habari kwamba Wanasayansi wamekuja na ingizo jipya la kupendezesha sura.

Wanasayansi hao wanasema wamegundua kuwa ute wa Konokono hulainisha ngozi na mtumiaji huonekana mrembo zaidi akitumia ute huo kuliko vipodozi vya kawaida.

Wanasema, mtu akifika saloni konokono huchukuliwa na kuwekwa usoni kisha huanza kutembea na hatimaye ngozi ya mtu husika baada ya muda mfupi hulainika na kuwa nyororo.

Kwa sasa ute wa konokono unatumika na wataalamu wa urembo kutengeneza bidhaa za ngozi na wanadada wengi wametokea kupenda huduma hiyo.

#Niambie endapo mwenza wako ‘akikuibukia’ kuomba salio ili akapate huduma kama hii…. utamsapoti?

Kocha Minziro aipa kongole Geita Gold
Arme Slot aikataa Tottenham Hotspur hadharani