Mshambuliaji  wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Emmanuel Ulimwengu yuko fiti kabisa sasa na atakuja nchini kuichezea nchi yake mechi mbili za Kundi G kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani.

Na klabu yake, Tout Puissant Mazembe imemruhusu kuja Dar es Salaam kuugana na Taifa Stars kwa ajili ya michezo miwili ya nyumbani na ugenini dhidi ya Chad.

TPM imemuambia Ulimwengu, maarufu kama Rambo mbele ya mashabiki wa Lubumbashi kwamba atakwenda Dar es Salaam mara tu baada ya mchezo wa marudiano wa Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya St George ya Ethiopia Jumapili ya Machi 20 mjini Lubumbashi.

Taifa Stars watakuwa wageni wa Chad Jumatano ya Machi 23 mjini N’Djamena, kabla ya timu hizo kurudiana Machi 28 mjini Dar es Salaam.

Ulimwengu akiumia mguu akiichezea Mazembe dhidi ya St Eloi Lupopo Februari 17, mwaka huu katika Ligi Kuu ya DRC timu hizo zikitoka sare ya 0-0 na akacheza kwa dakika 12 za mwisho huku akichechemea Februari 20 katika mchezo wa Super Cup ya CAF dhidi ya Etoile du Sahel ya Tunisia mjini Lubumbashi, wenyeji wakishinda 2-1.

Chanzo; Bin Zubeiry

Real Madird Kusaka Heshima Barani Ulaya Leo
Mata Awaomba Radhi Mashabiki Wake