Waziri wa Nishati, Januari Makamba amesema kasi ya ujenzi wa mradi wa umeme katika Bwawa la Mwalimu Nyerere – JNHPP, ni ya kuridhisha na sasa maji yamefika mita za ujazo Bilioni sita.
Waziri Makamba ameyasema hayo kufuatia ziara yake ya hivi karibuni katika eneo la mradi na kuongeza kuwa, kina cha maji kimebakiza urefu wa mita 13 pekee, kufikia kiwango cha kuzungusha mitambo ya kufua umeme.
“Kazi ya kuunganisha mitambo ya kufua umeme inaendelea na kwa mvua zilizonyesha maji yameingia mengi kuliko yalioleta mafuriko 2019/20 hivyo tuta la Bwawa hili na kazi ya kujaza maji vimesaidia kuepusha mafuriko Rufiji.” alisema na kuongeza kuwa ujenzi wa Bwawa umefikia asilimia 85.06.
Aidha, Waziri Makamba amebainisha kuwa Mvua zilizonyesha, zimepeleka Maji kuingia kwa wingi kuliko yale yaliyoleta mafuriko 2019/20 ambapo tuta la Bwawa hilo na kazi ya kujaza maji, vimesaidia kuepusha mafuriko Rufiji.
#KuelekeaUmemeWaUhakika